Muigizaji
wa Bongo movie Jacqueline Wolper amemtupia Dongo zito Sarah baada ya
habari zake za kumtosa Harmonize na kumchukua Bodyguard wa Diamond,
Mwarabu Fighter.
Siku
tatu zilizopita stori iliyotrend kupita zote ni ya mpenzi wa Harmonize
Sarah kumtosa mpenzi wake na kumchukua Mwarabu Fighter.
Inasemekana
Sarah amekufa ameoza kwa Mwarabu kiasi ya kwamba anamuhudumia ipasavyo
yaani kampangishia hadi nyumba yaani zile huduma zozote alizokuwa
anapata Harmonize zimehamia kwa Mwarabu.
Kama
utakumbuka Kuwa Sarah na Wolper ni maadui wakubwa na kisa kikiwa ni
penzi la Harmonize na juzi tu wametoka kumgombania Harmonize.
Baada
ya tetesi hizo za usaliti kusambaa mitandaoni Sam Misago Tv walimsaka
Wolper na kumuuliza nini maoni yake juu ya ishu hii kumuhusu Sarah na
Wolper ameishia kumtupia dongo zito Sarah:
"Duh
iyo ishu mbona ni exclusive kabisa sijaisikia lakini freshi tu mbona
yule demu ni Mlezi wa wana labda kachoka kumlea mwana kaamua kumchukua
mwana mwingine freshi tu”.
Bifu la Wolper na Sarah lilianza baada ya Sarah kuanza kuchepuka na Harmonize wakati Wolper yupo Kwenye Mahusiano na Harmonize.
Comments