Waziri asema si kila mtu ana mamlaka kuagiza upimaji DNA.....Atoa Maagizo Mazito Kwa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu.
Serikali
imekataza Mamlaka ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali
(GCLA), kuruhusu watu au taasisi zisizo na mamlaka kisheria kuwaamuru
kupima sampuli za vinasaba (DNA).
Agizo
hilo lilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile,
katika hafla ya uzinduzi wa Bodi Tendaji ya GCLA.
Bodi
hiyo ina wajumbe saba kutoka Wizara za Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto; Mambo ya Ndani ya Nchi, Katiba na Sheria na
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Dk.
Ndugulile ameitaka mamlaka hiyo kutoa elimu kwa jamii kuhusu majukumu
ya mamlaka hiyo, ili kuepuka watu au taasisi kutoa maagizo juu kwa
mamlaka hiyo kinyume cha sheria na taratibu.
“Tusiamini
kila mtu anajua utaratibu. Tunaweza sasa kuja kuvumbua mambo ambayo
hayapo. Si kila mtu anaweza kuamrisha Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu
wa Serikali kuchukua vipimo vya DNA, si hivyo kuna taratibu zake,”
alisema.
Alisema
lazima watu waelezwe taratibu zikoje, nani anawajibika kwenda kupeleka
sampuli na nani ana wajibu huo kwa sababu majukumu yake ni ya kisheria.
Dk.
Ndugulile alisema katika siku za karibuni suala la kupima vinasaba
limezungumziwa sana hali ambayo imezua mkanganyiko kwa jamii, hivyo
kuitaka mamlaka hiyo kutimiza wajibu wa kutoa elimu.
Pamoja
na kutokumtaja mtu aliyetoa amri ya watu kupimwa DNA, hivi karibuni
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliwaita watu waliodaiwa
kutelekeza watoto kujitokeza.
Baadhi
ya watu hao walijitokeza, lakini 90 kati ya wanaume hao, waliwakana
watoto waliodaiwa kuwa wamewatelekeza na kutaka waende wakapimwe DNA
katika maabara ya Mkemia Mkuu ili kumaliza utata huo.
Katika
hatua nyingine, Dk. Ndugulile aliitaka taasisi hiyo kuwa na mkaguzi wa
kimataifa wa ubora wa sampuli wanazopima, ili zikubalike kitaifa na
kimataifa.
“Lazima
muwe na mkaguzi wa kimataifa wa kuthibitisha kile mlichopima kwa sababu
taasisi hii ina majukumu ya kisheria ya kuamua ukweli kuhusu sampuli
iliyopimwa. Mkisema huu ni unga wa mahindi ilhali tunaona ni dawa za
kulevya hatuwezi kupinga,” alisema.
Pia
aliitaka mamlaka hiyo kutoa majibu kwa wakati, ili kupunguza kesi
zilizopo mahakamani zinazosubiri majibu ya maabara hayo.Alisema, ili
kutekeleza agizo hilo, amewataka kuandaa mikataba inayoonyesha kazi
itakamilika kwa muda gani pindi wanapopokea sampuli.
“Utakumbuka
kuna wakati kesi zilirundikana katika mahakama zetu hivyo mnatakiwa
kufanya kazi kwa haraka na kwa wakati na muwe na mikataba inayoonyesha
kazi itakamilika kwa muda gani,” alisema.
Pia
aliwataka kuwatambua wale wote wanaojihusisha shughuli za kemikali
nchini wakiwamo, wauzaji, wanunuzi na wanaozitumia kwa ajili ya
kupunguza matukio ya uhalifu nchini.
Kadhalika
aliwataka kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi na
Mazingira (NEMC) kuthibiti majitaka katika viwanda, ili kuepusha madhara
kwa watu.
“Sijawasikia
mkipima maji taka yanayotiririka viwandani mmekaa kimya kama si wajibu
wenu, hakikisheni mnashirikiana nao na kuchukua sampuli nyie wenyewe
mpime na mtoe majibu,” alisema.
Naye
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Fidelice Mafumiko, alisema GCLA
inakabiliwa na uhaba wa watumishi takribani 200 na pia uchakavu wa
mitambo ya kimaabara.
Dk.
Mafumuko pia alisema fedha za bajeti ya serikali ya mwaka 2017/18
zilizotengwa kwa ajili ya kununua mitambo na vifaa vya maabara hiyo
hazijatoka hadi sasa hali ambayo inawafanya kushindwa kutekeleza
majukumu yako kikamilifu.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Ester Jason, aliahidi kuisumbua wizara
hiyo kuhusu kutekeleza majukumu ya mamlaka ikiwa ni pamoja na kutoa
fedha mapema iwezekanayo.
Mpekuzi.
Comments