Wanaonufaika na mradi wa TASSAF watoa shukurani kwa matunda wanayofaidika nayo.

Related imageWananchi wanaofaidika na mpango wa tassaf wa kusaidia kaya maskini Zanzibar  wameishukuru serikali kwa hatua ya kuwasaidia  mradi  ambao umewawezesha kujikwamua na  umaskini kwani hivi sasa wameweza kujikimu na hali ngumu ya maisha kupitia tassaf.

Wakizungumza  Baadhi ya Wananchi wanaofaidika na mradi wa tassaf Mkoa wa Kaskazini Unguja Shehia ya Mkataleni wamesema  mradi wa tassaf ni wa kupigiwa mfano katika kuinua maisha ya wanyonge  kwani wameweza kuwasaidia  watoto wa maskini kuweza kusoma na  wazazi  kuweza kujiajiri wenyewe kupitia  miradi mbalimbali waliyoianzisha  kujiajiri.

Kwaupande wake Mratibu kutoka tassaf upande wa unguja Makame Ali Haji amesema  Zanzibar zipo kaya  ambazo zilikuwa zinaishi katika  mazingira  magumu na  hatarishi , Serikali  kwa kuliona  ikaamua kwa makusudi kuwasaidia wananchi wake kuondokana na maisha hayo.

Amesema  kuwa ujio wa mradi wa tassaf kwa kuzisaidia kaya maskini umeweza kuwainua wananchi wengi kwenye wilaya mbalimbali za unguja na pemba  na wananchi wengi wameweza kunufaika na kuweza kujikimu kimaisha.

Kwaupande wake Sheha wa Shehia ya Mkataleni Sharifu Ali Makame amesema zaidi ya wananchi 216 katika shehia yake wananufaika na mradi huo wa kusaidia kaya maskini na wameweza kupiga hatua wananchi katika nyanja za kimaendeleo.

Sheha huyo ameiyomba serikali kuzidisha  kasi ya kuwasaidia  wananchi wengine ambao bado hawajaingiwa katika mradi huo ili nao waweze kujikwamua na hali ngumu ya maisha.

Zanzibar24

Comments