Kampuni
zinazotengeneza vifaa vya ujenzi zimeshauriwa kutumia fursa ya kufanya
biashara hususani katika kipindi hiki ambacho serikali inahamia Dodoma.
Ushauri
huo ulitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi
wakati alipokuwa akizungumzia juu ya maandalizi ya maonyesho kwa kampuni
zinazotengeneza vifaa vya ujenzi na samani za ndani pamoja na wadau wa
sekta ya ujenzi.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini hapa amezitaka kampuni hizo kutumia fursa
ya ujio wa makao makuu kwa kujitambua, ili mashirika, taasisi na watu
binafsi wanaojenga Dodoma wafahamu ni bidhaa gani bora kwa ajili ya
ujenzi.
Maonyesho
hayo yanafahamika kama Dodoma Builders Expo 2018, na alisisitiza kwamba
fursa hiyo ni kubwa na wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi waitumie
kuonyesha bidhaa bora.
Kunambi
alisema ni kosa kulifananisha jiji la Dodoma na mikoa mingine nchini
kwani linatakiwa kufananishwa na Jiji la Nairobi Kenya na Pretoria
Afrika ya Kusini.
Kwa
upande wake mratibu wa maonyesho hayo, Victor Simon alisema katika Jiji
la Dodoma kuna vibarua na mafundi ambao wote wanachangamoto
zinazofanana.
Mratibu
huyo aliwataka makandarasi wa jiji hilo kuwatumia mafundi na vibarua wa
Dodoma, na kuacha tabia ya kutumia wale wa kutoka maeneo mengine.
Alisema
maonyesho hayo pia yanalenga kuwatambulisha na kuwaibua mafundi na
vibarua na wanatarajia kuongeza ujuzi na kukuza vipato.
Mpekuzi.
Comments