SMZ imesema kuwa imejipanga vyema katika kuhakikisha inazuia biashara za magendo.

Serikali  yamapinduzi  ya  zanzibar  imesema  kuwa  imejipanga  vyema  katika  kuhakikisha  inaziba njia  za  uingizaji  na utowaji  wa  bidhaa  kinyume  na  utaratibu  ndani  ya  kisiwa  cha  zanzibar. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi boti mbili za mwendo kasi kwa kikosi cha kuzuwiya magendo zanzibar na kikosi cha uwokozi  zanzibar ambapo  boti  hizo  zimetolewa  na  taasisi ya rom  solution Inayojihusisha na  masuala ya ulinzi zanzibar waziri  wa  nchi  ofisiya  rais  serikali  za  mitaa  na  idara  maaalum  za  SMZ Haji  Omari  Kheri  huko bandrini  mjini  zanzibar.

Amesema  kuwasili  kwa  boti  hizo  za  kisasa  kutapelekea  ufanisi  na  utekelezaji wa majumkumu  katika  vikosi vya  usalama hususani  masuala  ya  ulinzi  na  uwokozi  katika maeneo  ya  bahari.

Aidha  mkuu  wa  mkoa  mjini  magharibi  ayoub  mohammed  mahmoud  amesema  zanzibar imejenga historia kwa kupokea boti  hizo  hususani  ya  uwokozi  katika  mkoa  wake.

Wakizungumza  mara  baada  ya  kukabidhiwa  boti  hizo  wakuu wa  vikosi  vya  kmkmk  na zima  moto    wamesema  kukabidhiwa  kwa  boti  hizo  kutajengea  uwezo  kwa  watendaji  wa  taasisi  zao  kutekeleza  majukumu  yao  kwa  ufanisi  na kuondosha  changamoto  zinazowakabili  katika  masuala  ya  ulinzui  na  uwokozi.
Makabidhiano ya boti  hizo yametolewa  na  kampuni  ya Rom  solution  ikiwa  ni  mwendelezo  wa  mkataba  ulipo  kati  ya serikali ya mapinduzi  ya  zanzibar kupitia  wizara  ya  nchi  ofisi  ya  rais  tawala  za  mikoa  idatra  malaum  za  smz  katika kuimarisah  ulinzi  na  usalama. 

 
Zanzibar24.

Comments