
Akizungumza katika mahafali ya wanafunzi
wa kidatu cha sita wa skuli ya sekondari ya Jang’ombe ,katibu tawala wa
mkoa wa Mjini Magharibi Hamida Mussa khamis amesema Serikali inatambua
matatizo yanayowakabili wanafunzi na tayari ipo katika hatua ya
kuyatatua matatizo hayo.
Amesema Serikali ya Mkoa huo kwa
kushirikiana na wadau wa maendeleo pamoja na watu binafsi imekusudia
kuimarisha sekta ya elimu ili kuweza kuzalisha wataalamu
watakayoiwezesha serilikali ya Zanzibar kufikia uchumi wa Viwanda.
Katibu tawala huyo pia amechukua fursa hiyo
kuwataka wananfunzi kuwa na nidhamu wakiwa madarasani ili kuengeza
ufaulu katika mitihani yao wanayotarajiwa kufanya may7 mwaka huu.
Aidha ametowa wito kwa wanafunzi kuendelea
kusoma kwa bidii ili kupatia ufumbuzi tatizo la wataalamu wa fani
mbalimbali Nchini ikiwemo wataalamu wa sekta ya Afya na Elimu ambayo
ina mahitaji makubwa kwa wananchi.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu Mstaafu wa
Skuli ya Sekondari ya Jang’ombe Suleiman Mbarouk amesema ili wanafunzi
waweze kufaulu mitihani yao ni vyema kwa walimu kujua wajibu wao katika
kuwapatiwa wanafunzi elimu inayoendana na mahitajitaji yao.
Amesema wanafunzi wana mwamko mkubwa wa
kusoma masomo yao ila wanarejeshwa nyuma na baadhi ya matatizo
wanayokumbana nayo ikiwemo uhaba wa vifaaa vya skuli na walimu wa
kutosha jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo yao.
Aidha ametowa wito kwa wazazi na walezi
kuimarisha marikiano kati yao na walimu ili kuwawezesha wanafunzi
kufikia malengo waliyoyakusudia katika masomo.
Nae afisa Elimu wa Mkoa wa khatib Tabia
ameiomba Bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu kuangalia namna ya kuwasaidia
wananfunzi wa masomo ya sanaa kupata mikopo ili waweze kujiendeleza
kitaaluma.
Amesema wananfunzi wengi wanashindwa
kuendelea masomo yao kutoka na kukabiliwa na ugumu wa maisha katika
familia zao hivyo watakapo patiwa mikopo itawawezesha kufikia malengo
waliyoyakusudia pamoja na kuengeza wataalamu wa masomo hayo Nchini.

Awali katika risala ya wanafunzi
iliyosomwa na Zulfa Sharif wanafunzi wa skuli hiyo wamesema mbali na
kusoma kwa bidii washindwa kufanya vizuri katika masomo yao kutoka na
kukabiliwa na matatizo ya uhaba wa Vitabu,Vifaa vya Maabara na
madawati.

Aidha wametowa wito kwa serikali ya Mkoa wa
Mjini Mgahribi kupitia kampeni ya MIMI NA WEWE kuwajengea holi
litakalotumika kwa shughuli za skuli na shughuli nyenginezo ambazo
zinachangia mapato ya kuiendeleza skuli hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugeni wa
Sekondari ,Afisa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Muhammed Aboud amesema Wizara itaendeendelea kuimarisha miundombinu ya
skuli zote za Zanzibar ikiwemo upatikanaji wa vifaa vya maabara na
Vitabu vya kusomea.
Zanzibar24.
Comments