SHIRIKA la Meli na Uwakala Zanzibar,
lina mpango wa kununua meli nyengine mpya ya abiria na mizigo ili
kuondosha changamoto ya usafiri wa abiria, baada ya kukamilika ununuzi
wa meli ya mafuta.
Mkurugenzi wa shirika hilo, Ahmada Vuai, alieleza hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, ofisini kwake Malindi.
Alisema lengo la ununuzi wa meli hiyo ni kuondosha changamoto ya usafiri wa abiria kati ya Pemba, Unguja na Dar es Salaam.
Kuhusu meli ya Mv Mapinduzi II, alisema
inaendelea na matengenezo na inatarajiwa kuanza safari katika kipindi
cha mwezi mtukufu wa ramadhani.
Alisema shirika linaelewa changamoto zinazowakumba abiria lakini waliwaomba kuendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki.
Alisema ili kuhakikisha huduma ya
usafiri inakuwa endelevu serikali kwa kushirikiana na shirika hilo
imekusudia kuifanyia matengenezo makubwa meli ya Mv Maendeleo ili
iendelee kutoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo.
Zanzibarleo.
Comments