Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amewajibu watanzania ambao wanakosoa mpango wa serikali wa kuwapeleka
walimu wa sekondari kufundisha shule ya msingi.
Rais
Magufuli amesema kuwa kitendo hicho ni cha kawaida kwani hakiadhiri
mishahara yao bali kinawapa muda mwingi walimu hao kufanya kazi nyingine
za ziada.
“Wakati wa Nyerere walikuwa wanachukuliwa walimu wa UPE kwenda kufundisha shule za msingi. Sasa tunachukua wenye digrii.
"Kikubwa kinachoangaliwa ni mshahara wake tu.. Kwa sababu mshahara unapimwa si kwa vile unafundisha shule ya msingi, ni kutokana na Qualification zako.
"Tena kule ni kurahisi tu unaweza kufanya na mambo yako mengine.“alisema Rais Magufuli jana Mei 2, 2018 wakati akizungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, kilichopo mkoani Iringa.

Magufuli alitolea mfano wa nchi zinazotumia Maprofesa kufundisha shule
ya msingi; “Ukienda nchi za Scandinavia utakuta maprofesa ndiyo
wanafundisha chekechea, na mishahara yao ni mikubwa kuliko wanaofundisha
chuo kikuu. Just mind set.”
Mwezi
Februari mwaka huu serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma ilitangaza kuwa baadhi ya walimu wa masomo ya sanaa
kutoka shule za sekondari watapelekwa shule za msingi ili kukidhi
mahitaji.
Mpekuzi.
Comments