Rais Magufuli Anusa Ufisadi wa Bilioni 8 Ukumbi wa Chuo cha Mkwawa....Atoa Maagizo Mazito Kwa Vyombo vya Dola.
Rais John Magufuli amefichua siri ya
kukataa kuweka jiwe la msingi katika ukumbi wa jengo lililopo katika
Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa mkoani Iringa akisema limejengwa
kifisadi kwa Sh 8bilioni.
Rais
ameeleza hayo jana, Mei 2, 2018 wakati akizungumza na wafanyakazi na
wanafunzi wa chuo hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani humo.
"Muda
mwingine tuambizane ukweli Chuo cha Mkwawa kimeniangusha, ndio maana
nilikataa kuja kuweka jiwe la msingi katika lile jengo. Siwezi kuweka
jiwe la msingi katika jengo la kifisadi.
"Nikitoka
hapa nitakwenda kulikagua. Nilitegemea chuo hiki kitasimamia value of
money (thamani ya fedha), kwa sababu kuna wasomi lakini tofauti."
Rais
Magufuli alitumia nafasi hiyo kuviagiza vyombo vya dola kuhakikisha
wanawachukulia hatua wale wote waliohusika katika mchakato huo hata kama
wamestaafu, watafutwe waliko.
"Mmeshindwa
kusimamia ujenzi wa lile jengo halafu leo mnaniomba mabweni? Nitaanzaje
kuwakubalia wakati huku mmeshindwa, siwezi. Vyombo vya dola na wizara
vifuatilie mkishindwa nitafuatilia.
Mpekuzi.
Comments