Mwanamuziki
wa Bongo fleva kutoka THT Nandy amekiri kuwa pamoja na mambo mengine
yote na maneno yakiwekwa pembeni staa wa Bongo fleva Ali Kiba
amemu-insipire sana kwa kinywaji chake.
Nandy
amekiri kuwa hatua aliyofikia Ali Kiba ya kuingiza kinywaji chake
mtaani ambayo ni Energy drink ni hatua kubwa sana ambayo imempa
changamoto hata yeye ya kufanya makubwa zaidi.
Kwenye
mahojiano aliyofanya na The Playlist ya Times, Nandy amekiri kuwa
kupitia Kiba ni vizuri wasanii wengi wakajifunza kuwa ni vizuri kuwekeza
nje ya muziki.
"Ameni-inspire
kwa kinywaji kwa sababu ukiangalia the package ya kinywaji chake jinsi
ilivyo ni project fulani ambayo ipo serious”.
Lakini
pia Nandy ameongelea uwekezaji wa wasanii wengine kama Diamond Platnumz
ambaye ni mmoja kati ya msanii Lakini pia mfanyabiashara.
"Tunaambiwa
nje ya kuimba tunatakiwa tuwekeze nje ya muziki wetu na ndicho hiki
kaka zetu wanafanya ukimuangalia kama Diamond, Alikiba ni vitu ambavyo
wanatuhamasisha”.
Kwa hivi sasa Nandy anafanya vizuri sana ngoma yake ya Ninogeshe inayoshika namba moja kwenye mtandao wa Youtube.
Comments