Mbunge
wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu
amesherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa gerezani huku familia yake
ikiisherehekea kwa kula chakula pamoja na watoto yatima wanaolelewa
katika Kituo cha Nuru, Uyole jijini Mbeya.
Sugu ambaye anafikisha umri wa miaka 46, alisherehekea siku hiyo akiwa gerezani ambako anatumikia kifungo cha miezi mitano.
Keki ya mbunge huyo ilipambwa kwa kuchorwa pingu, mnyororo na taswira ya chumba cha Magereza.
Sugu
alihukumiwa kifungo cha miezi mitano baada ya kukutwa na hatia ya kutoa
lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, Februari 26.
Mwingine
aliyehukumiwa kifungo hicho ni Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini, Emmanuel Masonga ambao wote wanatumikia kifungo cha miezi
mitano jela katika Gereza Kuu la Ruanda jijini hapa.
Jana,
uongozi wa Hoteli ya Desderia inayomikiliwa na Sugu ulisherehekea siku
hiyo pamoja na watoto yatima wa Kituo cha Nuru na kula nao chakula cha
pamoja.
Hilo ni agizo la Sugu kuendelea kuwa karibu na jamii ya wakazi wa Mbeya.
Mke
wa Sugu, Happiness Msonga alisema mumewe ndiye aliyeagiza siku ya
kuzaliwa kwake iadhimishwe pamoja na watoto yatima kwa kula nao chakula.
“Sugu
amesema anawapenda sana watoto na yupo pamoja nao licha ya kuwa yupo
gerezani, lakini kiroho yupo nao daima. Ameagiza jana kwa kuwa pia ni
Mei mosi, ni vyema tukashiriki sherehe hiyo na watoto yatima,” alisema.
Happiness
alisema Sugu kupitia uongozi wa hoteli yake wameanzisha mpango maalumu
wa kutembelea na kujumuika na vituo vya watoto yatima vilivyopo jijini
Mbeya kila mwisho wa mwezi kwa kuwapelekea chakula na misaada mingine.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Yatima cha Nuru-Uyole, Jarson Fihavango
alimshukuru mbunge huyo na uongozi mzima wa hoteli yake kwa kuwapelekea
chakula na misaada mingine watoto wanaowalea kituoni hapo.
“Tunajua
mbunge wetu alipatwa na matatizo, lakini pamoja na kwamba yupo
gerezani, lakini bado anawakumbuka wananchi wake. Sisi tunashukuru sana
kwa hiki alichotufanyia,” alisema Fihavango.
“Tunasema
aendelee na moyo huohuo na sisi tunamuombea. Hiki alichokifanya kina
baraka kubwa mbele za Mwenyezi Mungu, tunajua namna anavyoweza kumlipa.”
Mpekuzi.
Comments