
Mchungaji Msigwa amesema hayo jana May 02, 2018 usiku kwenye hafla
ndogo iliyoandaliwa na Rais Magufuli katika Ikulu ndogo mkoani Iringa
ambapo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa na dini.
“Mhe. Rais umekuwa ukisistiza katika hotuba zako kuwa
wewe hujali mambo ya vyama, na hili umedhirisha kuwa hujali mambo ya
vyama. Umesaidia sana hela za kutoka kwako zimekuja nyingi kama Mhe.
Mahiga kuna barabara nzuri katika kipindi chako umekuwa Rais, umejenga
barabara ya lami kutoka Mlandege hadi kwa mKuu wa Wilaya karibu bilioni
3.5 zimetumika.
Kuna stendi nzuri ya Ipogolo karibu shilingi bilioni 3
zimetumika, kuna maji kwa hiyo kuna vitu vingi vimetumika kwa kweli Mhe.
Rais hupendelei. Hela zinakuja hata kwa sisi ambao ni wa CHADEMA
unaleta hela, kwahiyo tunakupongeza sana.“amesema Mchungaji Msigwa mbele ya Rais Magufuli.
Rais Magufuli amekuwa mkoani Iringa kwa ziara ya siku tano ambapo leo
anatarajiwa kumaliza ziara yake na tayari ameshafungua miradi mikubwa
ukiwemo mradi wa barabara ya Iringa-Migoli-Fufu yenye kilometa 189 na
uliogharimu shilingi Bilioni 207.457.
Comments