Na Othman Ali Juma - Pemba
othmanalijuma8@gmail.com
Akina
mama wajawazito wanaopatiwa huduma katika kituo cha afya cha uondwe shehia ya
mtambwe kaskazini Pemba wanaendelea
kuteseka wakati wanapomaliza kujifungua kutokana na jiko la kupashia maji ya
moto(Heater) kuibiwa.
Jiko
hilo ambalo lilitumika kwa kupashia maji ya moto wajawazito pindi wanapomaliza kujifungu ili
waweze kujisafisha.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao wanawake hao wamesema ni
takribani wiki mbili sasa tokea kuibiwa kwa jiko hilo hivyo wanapohitaji huduma
hiyo hulazimika kuhodisha nyumba za jirani zilizopo karibu na hospitali hiyo hali ambayo inawapa usumbufu
mkubwa hususani nyakati za usiku.
Jaria Hamad Bakari
ambaye ni mkaazi jirani na hospitali hiyo amesema tokea kuibiwa kwa hita hiyo
kumekuwa na usumbufu mkubwa kwa mama wajawazito wanaotoka maeneo ya mbali pindi
wanapohitaji maji ya moto.
''Ilipokuwepo hita wazazi walikuwa hawataabiki
lakini tokea kuibowa umekuwa ni usumbufu kwa wazazi na hata
sisi wakaazi wa karibu na hospitali kwani usiku mkubwa kushajipumzisha
unakuta unagongewa wanataka wasaidiwe maji ya moto'' alisema
Jaria.
Mmoja miongoni mwa
wahudumu wa kituo hicho Hamida Juma Mohd amesema uwepo wa heater hiyo ilisaidia kwa kiwango
kikubwa kuboresha upatikanaji wa huduma kwa mama wajawazito lakini tokea
kuibiwa kwa hita hiyo kumepelekea kudorora kwa utolewaji wa huduma .
Aidha amesema kuwa ili
kupunguza usumbufu wanaoupata huwashauri mama wajawazito wanakuja kituoni
hapo kujifungua kuchukua maji yao katika
chupa.
Nae msimamizi wa kituo hicho Zainab Hassan Sheha
amesema mnamo majira ya saa kumi na mbili asubuhi alipokea taarifa hizo kwa
njia ya simu kutoka kwa mfanyakazi mwenzake
na wakati huo huo kuchukuwa uwamuzi wa kumpatia tarifa hizo DMO pamoja
na sheha na kumelekeza kuweka ripoti kituo cha polisi.
Sheha amesema kuwa
kutokana na kutokuwepo kwa mlinzi katika kituo chao kunachangia kwa kiasi
kikubwa kufanyika kwa hujuma hizo hivyo ameiyomba serikali kupitia wazara ya
afya kuwawekea mlizi hospitalini hapo.
Kwa upande wake sheha wa shehia hiyo Suleiman Bakar Khamis amesema
amelipokea tukio hilo kwa masikitiko
makubwa na kutoa wito kwa jamii yeyote aliyechukua jiko hilo kulirejesha mara
moja na kusema kuwa kuibiwa kwa hita hiyo si hasara kwa kwake tu bali ni
kwanajamii wote wa Mtambwe.
Akithibitisha kutokea
kwa tukio hilo kamanda wa Polisi wa mkoa wa kaskazini Pemba Haji Khamis Haji
amesema mnamo tarehe 26 majira ya asubuhi waliripotewa tukio hilo na hadi sasa wanaendelea na uchunguzi kubaini ni nani
aliyehusika na tukio hilo.
Kamanda haji ametoa wito
kwa wanajamii wa Mtambwe kushirikiana na
jeshi la polisi kwa kulipatia taarifa ili kuhakikisha wanafanikiwa kumkamata
aliyetenda kosa hilo.
Comments