Naibu Katibu wa CCM Zanzibar, Abdalla Juma Maabodi alieleza hayo alipokua akizungumza na wanaCCM wa jimbo hilo kwenye hafla iliyofanyika katika tawi la Rahaleo.
Alisema chama kinahitaji maendeleo, umoja na mshikamano na sio kuwagawa viongozi kwa ajili ya maslahi binfasi ya watu wachache.
Naibu huyo alisema, iwapo viongozi hao watakuwa hawafanyikazi kwa kushirikiana ni vigumu kuweza kutekeleza miradi ya maendeleo, hasa ikizingatiwa fedha za mfuko wa jimbo haziwezi kukidhi mahitaji yote ya wananchi.
“Viongozi hao watakapofanyakazi kwa pamoja utapatikana ufanisi bora wa utekelezaji wa kazi zao, acheni tabia mbaya za kufitinisha viongozi”, alisema.
Alisema makundi ndani ya chama yanaleta shida kwa viongozi na sio wakati wake huku akiwataka kuwa wastaarabu na kuondoa tofauti kwani wote wanajenga nyumba moja.
“Nafahamu vizuri baadhi ya tabia za watu kwani nilipokua mbunge yote hayo yamenifika, nawaombeni tuache tabia hiyo sio njema na mfahamu wakati wa “iena iena” umemaliza tuimarishe chama chetu ili tushinde kwa kishindo ifike 2020”, alisema.
Kuhusu mali za chama alisema, lazima kuwe na utaratibu maalumu wa matumizi ya fedha zinazotokana na rasilimali ya chama kwani hatovumiliwa mtu yoyote atakaetafuna au kutumia fedha hizo kinyume na utaratibu.
Wakati huo huo, aliwaagiza makatibu wenezi wa chama hicho kuhakikisha wanasimamia madarasa ya itikadi kwa vijana, kwani yatasaidia kuwajengea uzalendo sambamba na kuitambua itikadi ya chama.
Kwa upande wake Mwenyekiti CCM, wilaya ya Mjini Juma Faki, alisema suala la vijana kujifunza itikadi ni jambo la msingi na roho ya chama, hivyo lazima kuwa wavumilivu kusoma madarasa hayo ambayo yatawasaidia kutambua historia ya nchi yao.
Zanzibarleo.
Comments