Kikosi kamili Hawa ndio wachezaji 23 Brazil, walioteuliwa kushiriki Kombe la Dunia.

Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Adenor Leonardo Bacchi maarufu kama Tite ametangaza majina 23 ya mwisho kwaajili ya fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kuanza June 14, 2018 nchini Urusi.
Brazil ambayo ipo E na timu za Costa Rica, Serbia na Switzerland, itacheza mechi yake ya kwanza Jumapili ya Juni 17. Nyota wa PSG Neymar ambaye ametoka majeruhi hivi karibuni ameitwa huku mlinzi Dan Alves akiachwa baada ya kuumia wiki iliyopita.

Mabingwa wa England Man City ndio timu ambayo imetoa wachezaji wengi kwenye kikosi hicho ikianza na mlinda mlango Ederson, mlinzi Danilo, kiungo Fernandinho na mshambuliaji Gabriel Jesus.
Kikosi Kamili:
Makipa: Alisson (Roma), Ederson (Manchester City), Cassio (Corinthians).

Walinzi: Danilo (Manchester City), Fagner (Corinthians), Marcelo (Real Madrid), Filipe Luis (Atletico Madrid), Thiago Silva, Marquinhos (both PSG), Miranda (Inter Milan), Pedro Geromel (Gremio).

Viungo: Casemiro (Real Madrid), Fernandinho (Manchester City), Paulinho (Barcelona), Fred (Shakhtar Donetsk), Renato Augusto (Beijing Guoan), Philippe Coutinho (Barcelona), Willian (Chelsea), Douglas Costa (Juventus).

Washambuliaji: Neymar (PSG), Taison (Shakhtar Donetsk), Gabriel Jesus (Manchester City), Roberto Firmino (Liverpool).

Comments