Kifungo cha miaka 5 chamkuta msichana aliemuiba mtoto wa mwezi mmoja Fuoni.

Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe imemuhukumu mshtakiwa Aisha Ngumbi Deus mwenye umri wa miaka 19 mkaazi wa Mwanza Tanzania Bara  kwakoso la wizi wamtoto na kuekwa chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka mitano.

Mnamo tarehe 5 mwezi wa 5 mwaka 2018 majira ya saa 3 za asubuhi Mtaa wa Fuoni Jitimai ambapo alimuiba mtoto wakiume mwenye umri wa mwaka mmoja nakukamatwa katika bandari ya Malindi Mjini Zanzibar kwani alikua akitaka kutoroka nae kuelekea jijini dar es salaam.

Aliposomewa kesi hiyo Mahakamani hapo amekiri kosa hilo na Mahakama imemtia hatiani kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 5 ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kamahizo.
Zanzibar24.

Comments