Kanisa
Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, limewapiga marufuku wanawake wajawazito
kuvaa shela wakati wa kufunga ndoa kwa madai vazi hilo ni alama ya
ubikira kwa mwanamke na sio vinginevyo.
Hayo
yamesemwa na Paroko Msaidizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresa, Padre
Festus Mangwangi wakati akiweka mkazo juu ya tamko lililotolewa na
Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Isaack Amani, wakati akiadhimisha misa ya
shukrani iliyofanyika Jumapili iliyopita, baada ya kuteuliwa kwake na
Baba Mtakatifu Francis kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo.
Kabla ya uteuzi huo uliotangazwa Desemba 27 mwaka 2017, Askofu Mkuu Amani alikuwa Askofu wa Jimbo la Moshi na kusema haitakiwi kwa mwanamke yeyote ambaye anajijua ni mjamzito kuvaa shela kipindi anafunga ndoa kwa kuwa vazi hilo linavaliwa na mwanamke asiyemjua mwanaume (bikra).
Kabla ya uteuzi huo uliotangazwa Desemba 27 mwaka 2017, Askofu Mkuu Amani alikuwa Askofu wa Jimbo la Moshi na kusema haitakiwi kwa mwanamke yeyote ambaye anajijua ni mjamzito kuvaa shela kipindi anafunga ndoa kwa kuwa vazi hilo linavaliwa na mwanamke asiyemjua mwanaume (bikra).
Aidha,
Padre Festus Mangwangi amewataka wazazi kuwafundisha watoto wao wa kike
kutunza miili yao na kuishi maisha ya kimaadili hadi watakapopata wenza
wa kufunga nao ndoa na hapo ndipo alama ya shela itakapoonekana umuhimu
wake.
"Tamko
la Askofu Mkuu linatekelezwa kwa kuwaeleza maharusi watarajiwa
wanapokwenda kupata mafundisho ya ndoa kwa katekista na baadaye padre,
kuwa kama ni wajawazito basi wasivae shela na hata wale wanaowajua
wanaume pia wanashauriwa wasivae", amesema Padre Festus.
Pamoja
na hayo, Padre Festus ameendelea kwa kusema "wanaojitambua kuwa si
bikira, hawavai shela, lakini wako wanaojificha na kuvaa shela, hii
inakuwa sawa na kudanganya".
Kwa
upande mwingine, Padre Festus amesema endapo atatokea mtu akadanganya
na kuvaa shela wakati tayari anamjua mwanaume au kuwa mjamzito basi
atakuwa anafanya utovu wa nidhamu.
Mpekuzi.
Comments