
Na Othman Ali Juma - Pemba
othmanalijuma8@gmail.com
Wananchi wa shehia ya mtambwe kaskazini Pemba wanahofu
ya kusimama kwa huduma za usafiri na shughuli
zao za kiuchumi kutokana na kalafati ya
barabara yao kughariki hali inayowapa wasi wasi kuwa muda wowote kutoka sasa njia hiyo inaweza
kukatika.
Wakizungumza huko kijijini kwao wananchi hao wamesema iwapo kama serikali
haitofanya juhudi za haraka kuzibiti daraja hiyo isiendelee kughariki muda
wowote kutoka sasa njia hiyo itakatika na kupelekea kusimama kwa huduma zao
muhimu za kimaisha.
Bakari Mwita Sheha na Omar Fakih Hassan wakaazi wa
kijiji cha uondwe wamesema kuwa asilimia 75 shughuli za kiuchumi za
wanamtabwe zinategemea uwepo wa barabara
hiyo hivyo iwapo kama haitofanyiwa matengenezo ya haraka itapelekea athari
kubwa kwa wanamtabwe.
''Kama daraja
ya mpaka njia itaachiwa ikatike basi kijiji cha uondwe na kele ambako ndio
kwenye standi za gari za mtambwe
watakosa huduma ya usafiri,pia itakuwa ni dhiki sana kwa wanachi kusafirisha
bidhaa zao kama vile ndizi,Muhogo na
nyenginezo kupeleka mjini ili kutafuta soko''.walisema wanakijiji hao.
Wamesema kuwa licha ya kusimama kwa shughuli za
kiuchumi lakini pia kutapelekea kutokupatikana kwa huduma muhimu za afya pindi
wanapolazimika kuzifuata maeneo mengine ambayo ni nje ya Mtambwe.
''Inapotokea mtu kaumwa na maradhi makubwa ambayo
hayawezekani kutibiwa hapa hutupasa kumpeleka Wete au Chake Chake jee njia
ikiachiwa ikatike tutamuduje kumpeleka huko''.walisema.
Akisibitisha kughariki kwa daraja hiyo ya Mpaka njia
Sheha wa shehia ya Mtabwe Kaskazini Suleiman Bakar Khamis amesema kwa takribani
wiki moja sasa tokea kughariki kwa kalafati hiyo na baada ya kuona hali inaendelea ndipo
alipoamua kupiga simu kunako husika na baada ya kuona hakuna hatua
waliyoichukua akamua kumpigia simu waziri.
''Baada ya kuona hali hii nilitoa taarifa akaja Dr.
Sira,Mh,Said Soud na Mh,Juma Ali Khatib wakaiyona hali ya njia ilivyo ila
nilipoona siku zinakwenda hakuna hatua waliyoichukua na hali ya njia inazidi
kuwa ngumu niliamua kumpigia Mh, waziri Dr, Sira Ubwa Mamboya.amesema sheha
huyo.
Aidha amesema ni jambo la aibu kuwa njia tokea ifunguliwe na
Mh, Rais hata miaka mitatu haijafika
sasa inaaza kukatika hivyo ametoa
wito kwa mainjiania wa ndani kuwa makini pindi wanapowakabidhi kazi makampuni kutoka nje kuhakikisha
wanajenga kwa viwango vinavyotakiwa ili kuepu kupoteza mamilioni ya pesa ambazo
zinahitajika kwa kuboresha huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake Afisa Mdhamini Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano
na Usafirishaji Hamad Ahmed Baucha
amesema kwa sasa wanaendelea na ujenzi wa kalafati hiyo na baada ya siku tatu
inatarajiwa kukamilika .
Baucha amewataka wanamtambwe kuwa wavumilivu kwa
kipindi hichi na kuwataka kutoa msaada wao pindi unapohitajika ili kukamilisha
ujenzi huo kwa muda uliopangwa.



Comments