Msanii
wa muziki wa Bongo Fleva kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka
sababu ya kutompa mkono Alikiba walipokutana katika msiba wa Agness
Gerald ‘Masogange’.
Muimbaji
huyo anayefanya vizuri na ngoma ‘Kwa Ngwaru’ ameiambia The Playlist ya
Times FM kuwa mambo yote yanayozungumzwa si ya kweli, bali walisalimiana
ila si kwa kushikana mikono.
“Unajua
asilimia kubwa ya watu wanaozungumza hawakuwa pale, unajua
unapomzungumzia Alikiba ni mtu ambaye amefanya muziki wetu upate heshima
kwa namna moja au nyingine, kama msanii namheshimu siwezi nikakutana na
mtu halafu nisimsalimie, sio kweli,” amesema na kuongeza:
“Kilichofanyika
ni kwamba Diamond kamsalimia kwa mkono, wamesamiliana kwa mkono. Mimi
nimekuja nimezunguka nikaona kwa kuwa Diamond kamsalimia kwa mkono,
kamgeuzia kiganja, mimi nikamsalimia kwa sauti tu, tukakaa pale
tukaendelea.” .
Comments