Mwanamuziki
wa Bongo fleva Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na mke
wake staa wa Bongo movie Irene Uwoya wanatafuta mtoto.
Uwoya
ambaye tayari ana mtoto mmoja Krish aliyezaa na marehemu Ndikumana
Kataut amedai yuko katika jitihada za kumtafutia Krish mdogo wake.
Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda,
kwa nyakati tofauti mastaa hao walifunguka kuwa, kwa kipindi hiki cha
mvua ndiyo muda sahihi wa kusaka mtoto hivyo wanalifanyia kazi suala
hilo kwa nguvu zao zote.
"Tupo
bize kidogo, tunasaka mtoto maana si unajua watu wanaangalia matunda ya
ndoa kwa jicho la tatu hivyo sisi tunaangaika na hilo sasa hivi,”
alisema Dogo Janja
Lakini
pia Uwoya naye alifunguka na kusema ni haki yake kumpatia mtoto mume
wake kama wanandoa lakini hasa hivi sasa anahitaji kumpa mdogo wake
Krish kwani ameshakuwa mkubwa.
"
Mke lazima amzalie mumewe na mimi na mume wangu sioni tunachosubiri kwa
sasa maana Krish ni mkaka mkubwa na anahitaji mdogo wake“.
Irene Uwoya na Dogo janja walifunga ndoa mwaka jana mwishoni.
Mpekuzi.
Comments