Aunty Ezekiel: Mchango wa Moze Kwangu ni Zaidi ya Pesa.

Siku ya May 1 , msanii wa bongo movie Aunty Ezekiel  alikuwa na press conference kwa ajili ya kuitangaza filamu yake mpya inayoitwa mama ambayo amemshirikisha mtoto wake wa kike Cookie.

Akiongea na waandishi wa habari, mama cookie anasema kuwa hakuamua kumshiriksha mume wake moze iyobo kwa sababu anaamini kabisa kila mtu amezaliwa na kipaji chake hivyo  anajua kuwa kuigza sio kazi ya Moze.

Aunty anasema kuwa aligundua kuwa mtoto wake ana kipaji lakini yeye kuwa na mahusiano na moze haimaanishai kuwa basi amlazimishe Moze kufanya movie wakati anajua kuwa moze hawezi kuigiza bali anaweza kucheza na ndio ilivyo hata kwake kuwa hawezi kucheza kwahiyo, kuna baadhi ya vitu kati ya ke na moze vitabai kuwa kama vilivyo.

"Mimi na Moze tuna mipaka, tumekuwa tukiihsi bila kuingiliana katika kazi,mimi siingiliani nae katika kazi zake, na yeye pia haingilii kwenye za kwangu hapana.

"Kwahiyo nisingependa kulazimisha kwa sababu eti ni mama aliyezaa nae, kwaio sijamshirikisha kwa sababu kipaji chake ni cha kucheza na sio kuigiza.

Moze kwangu ana mchango mkubwa sana , mchango wake ni mkubwa sana zaidi hata ya pesa kwa sababu ninapokuwa  nikipata ushauri wake na nikaufanyia kazi ndio unaokuwa unaniletea pesa."

Comments