
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa
Taasisi ya New Vision Consortium (NVCT) Pily Khamis Lapda, amesema
wanawake wengi hapa nchini wamekuwa wakifanya shughuli za ujasiriamali
kwa mazoea jambo linalopelekea kushindwa kufikia malengo yao ya kumiliki
mitaji mikubwa ya kibiashara.
Amesema zipo njia mbali mbali za kuwakomboa
wanawake kiuchumi zikiwemo kupenda na kuamini shughuli za ujasiriamali
kama nyenzo ya kujikomboa kiuchumi.
Amewashauri wanawake nchini kujiamini pindi
wanapoanzisha biashara zao sambamba na kujiwekea malengo ya kudumu ya
kibiashara yatakayowasaidia kumiliki mitaji mikubwa ya kibiashara.
Mkurugenzi huyo Pily, akizungumzia malengo
ya taasisi yake inayoendesha na kusimamia mafunzo ya kuyajengea uwezo wa
kitaaluma makundi mbali mbali ya kijamii ili kupata uwezo wa kutumia
ipasavyo fursa za ujasiriamali wenye maendeleo.
“Wanawake tuwe mstari wa mbele kujifunza
mbinu mbali mbali za kujikwamua kiuchumi, pia tujitume na kuwa wabunifu
katika biashara zetu ili nasi tuwe miongoni mwa wajasiriamali wa
kimataifa.”, amesema Mkurugenzi huyo.
Akitoa mada ya Uvumbuzi binafsi, mtaalamu
wa Saikolojia na maendeleo ya vijana, Joseph Mrindo amesema wanawake
waliopo katika sekta ya ujasiriamali wanatakiwa kuondokana na dhana ya
ujasiriamali mdogo mdogo kwani hali hiyo inasababisha kudumaa kiakili na
kushindwa kufikia malengo yao ya kumiliki biashara kunwa na makapuni.
Ameeleza kuwa Zanzibar ni sehemu muhimu
yenye fursa za kibiashara hivyo wanawake wanatakiwa kutumia nafasi hiyo
kujiongeza kibiashara.
Mtaalamu huyo, amewasihi wajasiriamali
kufuata maelekezo na mbinu mbali mbali za maendeleo ya kibiashara ili
wawe na mitaji mikubwa itakayowawezesha kupewa mikopo kwa wakati na
benki mbali mbali nchini.
Naye mshiriki wa mafunzo hayo, Munawar Sleiman Mbarouk amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili wajasiria mali ni ukosefu wa mitaji na ujuzi wa kufanya biashara zenye tija kwa mjasiria mali mmoja mmoja na vikundi.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanatolewa na
taasisi ya New vision consortium (NVCT)iliyopo Zanzibar na jumla ya
washiriki 200 kutoka taasisi binafsi na za umma wanapewa ujuzi huo wa
ujasiriamali.
Wadhamini wa mafunzo hayo ni pamoja na NMB, ZSSF, ZURA na IQUITY BANK.
![]() |
MKURUGENZI wa New vision consortium Pily Khamis Lapda(aliyekaa katikati) akifungua mafunzo ya siku mbili ya ujasiriamali kwa wanawake wa Zanzibar yaliyofanyika katika Skuli ya Haile-Sela-ssie. |

![]() |
BAADHI ya washiriki katika mafunzo hayo kutoka taasisi binafsi na za umma wakifuatilia kwa makini mada mbali mbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo, huko Skuli ya Haile-Sela-ssie. |
![]() |
MSHIRIKI wa mafunzo ambaye pia ni mjasiria mali kutoka U.WT. jimbo la Mwera Salama Mohamed Tahir akichangia mada ya uvumbuzi binafsi. |
Chanzo:ZANZIBAR24.
Comments