Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema hali ya mvua katika
maeneo mengi ya nchi itapungua kuanzia usiku wa leo Aprili 21, 2018.
Taarifa
ya TMA iliyotolewa jana imesema maeneo mengi ya nchi yanatarajiwa kuwa
na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi
vya jua.
Pia, TMA imesema maeneo mengine ya mikoa yatakuwa na
hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi
vya jua.
“Matazamio kwa siku ya Jumatatu Aprili 23, 2018, mvua
inatarajiwa kupungua katika maeneo mengi ya nchi,” imesema taarifa hiyo
ya TMA
Mpekuzi.
Comments