Serikali ya Z’bar yatoa onyo kali kwa wavuvi.

Makamu  wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  amesema Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria wavuvi watakao bainika wanatumia njia za  uvuvi haramu  wanapovua samaki baharini ili kulinda  samaki wadogo pamoja mazingira ya bahari.

Akizungumza katika Uzinduzi wa kituo cha utotoaji wa watoto wa samaki Hatchery huko Beit Ras amesema serikali imekuwa ikichukua juhudi mbalimbali katika  kukuza na kuimarisha sekta ya uvuvi  kwa  kutafuta wadau wa maendelo   kuekeza   katika sekta huu muhimu ambazo zinachangia katika kukuza na  kuongeza kasi ya ukuwaji wa uchumi  Zanzibar ikiwemo uvuvi,ufugaji,kilimo na utalii.

Amesema  uzinduzi wa kituo hicho cha kuzalishaji wa watoto wa samaki kitasaidia katika  kuwaondolea usumbufu  unaowapata wafugaji  katika upatikanaji wa watoto hao  kwani itaongeza  uzalishaji na kusema wakati umefika kwa wafugaji kubadilika na kuachana na ufugaji wa mazoea  ambao hauleti tija  kwao na taifa  na badala yake sasa  kufuga kwa ajili ya biashara na chakula ili  kuweze kupata soko ndani na nje ya nchi.

Aidha Balozi Seif amesema  endepo  wavuvi na wafugaji watautumia vyema mradi huo  utaweza kusaidia katika upatikanaji wa samaki wengi Zanzibar  ambao watachangia katika  kukuza na kuongeza  upatikanaji wa chakula  kiurahisi pamoja na kuongeza pato  la taifa  ambapo  awali sekta ya uvuvi inaongeza asilimia  10 katika pato la taifa.

Amesema lengo  kuu la kuanzishwa mradio huo katika  kituo hicho cha kutotolea  samaki ni  kurahisisha upatikanaji wa vifaranga vya samaki kwa wananchi ambao ni wafugaji  lakini  pia  ni  kuondoa tatizo la ajira kwa vijana  kwani kituo hicho kitakuwa na fursa  za upatikanaji  wa ajira pamoja na kupanua wigo katika sekta ya uvuvi kuweza kuleta maendeleo endelevu.

Hata hivyo Makamu wa Rais wa Zanzibar amesema  mashirika ya maendeleo yakiwemo  FAO  na Korea International Agency KOICA yamekuwa yanatoa michango mikubwa katika kukuza na kuendeleza Zanzibar  katika  sekta mbalimbali ambazo zinachangia  kuondoa umaskini na kuleta na kuleta maendeleo  ili kufikia uchumi wa kati  hivyo wananchi  hawana budi kuunga mkono juhudi na harakati zinazokuchukuwa na serikali pamoja na mashirika hayo ili Zanzibar iweze kuendelea.

Kwaupande wake Rais wa KOICA Mikyung Lee amesema  Wataendeleo kuiunga mkono Zanzibar katika kuharakisha maendeleo ya nchi  hiyo ambapo amesema mbali na kusaidia  katika sekta ya uvuvi na kilimo lakini pia  wataendelea kuisaidia Zanzibar katika sekta ya elimu ili kukuza vipaji kwa vijana ambapo wametenga  zaidi ya Dolla Million 15 za marekani ili kutumika katika sekta hiyo.

Lee amesema pia nchi ya  korea haita kuwa nyuma katika kuongeza juhudi kwenye  sekta ya afya kusaidia  kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu unaowasumbua wananchi na serikali kila ikifika kipindi cha mvua za masika ambapo amesema yote hayo ni kuiunga mkono serikali ya Zanzibar ili kuleta maendeleo nchini na  kuweza kufikia uchumi wakati.

Amesema Zanzibar inanafasi kubwa katika kukuza uchumi wake kutokana na kuwa na rasilimali nyingi  zenye kuuzika ndani na nje ya nchi ikiwemo rasilimali za baharini zinazovutia katika  kuongeza pato la taifa hivyo wananchi wazidi kuhamasika katika kutumia rasilimali hizo muhimu ili kupunguza umaskini.

Nae Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar Maryam Abdalla Mabodi amesema Vikundi mia moja na arobaini na nne zipo Zanzibar unguja na pemba zinavyofuga samaki  hivyo uwepo wa kituo cha kutotolea watoto wa samaki kitawasaidia pamoja na mabwawa matano yameanzishwa ili kuongeza kasi ya uzalishaji wa samaki.

Katibu Mkuu huyo amewataka wananchi wanaoishi karibu na bahari kutumia fursa za uwepo wa  bahari  katika  kuzalisha samaki wakiwemo kaa,kamba,chaza na majongoo ya pwani  ili kuweza  kujipatia kipato pamoja na kukuza sekta ya ufugaji na utalii.

Amesema lengo la uzalishaji huo wa watoto wa samaki ni kuzalisha zaidi ya watoto Elfu 10 kila mwaka ambapo jumla ya Dolla Million tatu laki mbili na Ishirini na nane elfu za Marekani zimetumika katika kuwezesha mradi huo wa kutotoa watoto wa samaki Zanzibar ambao ni mradi wa kwanza kwa ukubwa kwa Afrika.
 Zanzibar24ز

Comments