Maria Zakharova, ameyasema hayo kwenye mahojiano aliyofanyiwa na kanali ya tano ya televisheni ya Russia na kubainisha kuwa kutengwa Russia na Magharibi na kuzuia mashindano ya soka ya Kombe la Dunia yasifanyike ndilo lengo kuu linalofuatiliwa na nchi za Magharibi; lakini katu hazitofanikiwa kufikia lengo hilo.
Zakharova amesema ni jambo lisilowezekana kughairishwa mashindano ya soka ya dunia nchini Russia na kubainisha kwa lugha ya mafumbo kwamba: "jitihada zote zimeelekezwa kwenye mpira ili usije ukadundia kwenye uwanja wa soka wa Russia".
Mashindano ya 21 ya soka ya Kombe la Dunia yatafanyika kuanzia tarehe 14 Juni hadi Julai 15 nchini Russia.
Uhusiano wa kidiplomasia wa Russia na nchi za Magharibi umeharibika mno kutokana na kadhia ya kupewa sumu jasusi wa zamani wa Russia Sergei Skripal na binti yake Yulia nchini Uingereza.
Nchi karibu 30 zimewafukuza wanadiplomasia kadhaa wa Russia kuonyesha mshikamano na uungaji mkono wao kwa Uingereza katika sakata hilo, huku baadhi yao zikizungumzia pia uwezekano wa kususia mashindano ya soka ya Kombe ya Dunia yatakayofanyika nchini Russia..
chanzo:parstoday.
Comments