Mrembo
na muigizaji mkongwe kwenye tasnia ya filamu nchini Yvonne Cherrie
maarufu kama 'Monalisa' ameibuka mshindi kwenye tuzo za 'The African
Prestigious Awards' nchini Ghana akimbwaga mpinzani wake Lupita Nyong'o.
Katika
tuzo hizo zilizotolewa usiku wa kuamkia leo huko jijini Accra nchini
Ghana Monalisa ametwaa tuzo katika kipengele cha 'Best African Actress'.
Kwa mujibu wa tuzo hizo Monalisa sasa ndiye muigizaji bora wa kike barani Africa.
Monalisa
amethibitisha ushindi wake kupitia mtandao wa 'Instagram' ambapo
amepandisha picha akiwa na tuzo yake na kuandika ujumbe huu
''Tumeshindaaaaaaa narudi home na Tuzo za kutosha.Ahsante
Watanzania,Nawapenda mno''.
Kwa
ujumbe huo wa Monalisa unaashilia huenda pia kuna tuzo nyingine
wameshinda Watanzania ambao walikuwa wanawania vipengele mbalimbali
katika tuzo hizo kubwa za filamu nchini Ghana.
Watanzania
wengine waliokuwa wanawania ni King Majuto kipengele cha Mchekeshaji
Bora Afrika, Vicent Kigosi kipengele cha msanii Bora wa Kiume Afrika na
Mpiga picha Mahiri Moiz Hussein katika kipengele cha Mpiga Picha Bora
Afrika.
Comments