Wakati
Wabunge walikuwa wakichangia mapendekezo yao katika bajeti ya Waziri
Mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/19 Mbunge wa viti maalum CCM Hawa Mchafu
Chakoma ameishauri serikali kuanzisha namna bora ya mpango wa pensheni
kwa wazee waliolitumikia taifa.
Hawa
Mchafu alisema ;"Nashindwa kufahamu mfuko wa moja kwa moja ambao upo
kwa ajili ya wazee, muda umefika sasa ule mchakato wa pensheni kwa wazee
uje sasa ili kuweza kuwasaidia wazee wa taifa letu ambao kwa nafasi zao
walisaidia sana nchi yetu”
“Niipongeze
Serikali pia kwa kuanzisha miradi mbalimbali mikubwa ikiwemo ujenzi wa
bomba la mafuta, ujenzi wa viwanja vya ndege n.k ....ni wazi
itaambatana na upatikanaji wa ajira lakini niishauri Serikali ihakikishe
inafuatilia mikataba ya kazi kwa watanzania inayofanyika katika miradi
hiyo kwamaana kumekuwa na ukakasi mkubwa sana mikataba mingi
inaukiukwaji wa kisheria” –Hawa Mchafu
chanzo:Mpekuzi.
Comments