
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari ikuhusiana na matayarisho
hayo katibu mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Dk Vuai Iddi amesema
mashindano hayo yatajumuisha waendesha baskeli vijana kutoka nchi mbali
mbali za Afrika, hivyo amewata wananchi kujitokeza kushangilia pamoja na
kujionea uhondo wa mashindano hayo.
Amesea mashindano
hayo yatasaidia kuongeza idadi ya Watalii nchini na kuongeza pato la
taifa na wananchi mmoja mmoja pamoja na ongeza la ajira kwa vijana.
Rais wa vijana wa
Afrika Mashariki Fest Peter George Mzunda amesema lengo la mashindano
hayo ni kutangaza utalii pamoja na kuwapa fursa vijana kushiriki michezo
ya baskeli na kuamsha hamasa kwa vijana kupata ajira kupitia mchezo
huo.
Katibu mkuu wa
Chama cha baskeli Zanzibar amesema kwa upande wa chama chao wameshukuru
kupata nafasi ya kushiriki mchezo huo huku akisema wao wameweza kufanya
mchujo na kuwapata wachezaji kumi kwa ajili ya mashindano hayo.
Akizungumza kwa
niaba ya mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkuu wa Trafiki wa
Wilaya ya Mjini msaidizi wa Polisi Moh’d Talhata amesema kwa upande wa
Jeshi la Polisi limejipanga kiusalama ilikuhakikisha mashindano hayo
yanafanyika bila kuathiri shughuli za watu.
Mashindano hayo
ya Afrika Mashariki na kati kwa kilomita 60 yanatarajiwa kuanzia uwanja
wa Amani kupitia Mwera, Dunga, Jendele, Unguja Ukuu na kurejea kupitia
barabara ya Bungi, Fuoni, Mwanakwerekwe hadi uwanja wa Amani huku Mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub
Mohammed Mahamoud ambapo washiriki watatokea Tanzania bara, Kenya,
Uganda, Burundi na wenyeji Zanzibar huku mataifa mengine yakialikwa
katika Mashindano hayo wakiwemo Afrika ya Kusini, Zimbabwe, Zambia
na Swaziland.
Comments