Kampuni
inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es
Salaam, (UDART) imesitisha huduma zake kwa baadhi ya njia kuanzia saa
11:00 alfajiri tarehe 15/04/2018 kutokana na kufungwa kwa Barabara ya
Morogoro eneo la Jangwani kwa sababu ya mafuriko yaliyosababisha maji
kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi.
Aidha,
kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Kimara – Morroco, Kimara –
Magomeni Mapipa, na Gerezani – Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara
baada ya barabara kufunguliwa.
Hata hivyo, Kampuni hiyo kupitia kwa mkuu wa kitengo cha mawasiliano, Deus Bugaywa imeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
chanzo:Mpekuzi.
Comments