Kijana chipukizi wa Syria alitibua igizo la silaha za kemikali la nchi za Magharibi katika mji wa Duma.

Kijana chipukizi wa Syria alitibua igizo la silaha za kemikali la nchi za Magharibi katika mji wa DumaKijana chipukizi wa Kisyria mwenye umri wa miaka 11 aliyeonekana amejeruhiwa kutokana na shambulio la silaha za kemikali kwenye filamu iliyotengenezwa na wapinzani wa serikali ya Syria katika mji wa Duma amesema alishiriki kwenye filamu hiyo kwa ajili ya kupatiwa bidhaa za chakula.

Hassan Diab ameiambia kanali ya televisheni ya Russia 1: "siku ya kutayarisha igizo la hujuma ya gesi ya kemikali katika mji wa Duma tulikuwa tumekaa sehemu ya chini ya ardhi ndani ya nyumba tukiwa hatuna cha kukila; mara tukasikia sauti ya mtu anatuita kisha tukapelekwa hospitali; huko hospitalini watu kadhaa walitumwagia maji huku wakisema limetokea shambulio la gesi ya kemikali."
Baba wa mtoto huyo wa Kisyria amesema magaidi walimpatia Hassan bidhaa za chakula ikiwemo tende na mchele kama bahashishi kwa kushiriki kwenye igizo la hujuma ya silaha za kemikali.
Vasily Nebenzya, balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa mahojiano hayo aliyofanyiwa Hassan Diab yataonyeshwa katika kikao kijacho cha Baraza la Usalama la umoja huo kama hati ya ushahidi wa "upotoshaji" kuhusiana na shambulio hilo lenye kutia shaka.
Itakumbukwa kuwa Jumamosi ya tarehe 14 Aprili, Marekani, Ufaransa na Uingereza zilitumia propaganda zilizoenezwa kuhusiana na kadhia hiyo, na bila ya idihini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zikaishambulia Syria kwa mabomu ya ndege za kivita na makombora kwa madai eti jeshi la serikali limeshambulia mji wa Duma kwa gesi ya kemikali.
chanzo:parstoday.

Comments