Dogo Janja Aikingia Kifua Video ya Uchi ya Nandy.......Awachana Wasanii kwa Madai kuwa ni Wanafiki, Hawana Umoja.
Ikiwa
zimepita takribani siku mbili tokea mrembo Nandy kuomba radhi kutokana
na video yake ya faragha kusambaa mitandaoni, msanii Dogo Janja ameibuka
na kudai wasanii hawana umoja na wanafiki huwa wanafurahi sana kuona
mwenzao amepatwa na majanga ili mradi apotee katika tasnia.
Dogo
Janja ametoa kauli hiyo usiku wa kuamkia leo Aprili 15, 2018 kupitia
ukurasa wake maalumu wa kijamii na kusema anahisi anaweza kuchukiwa leo
hii na wasanii wenzake ila ni lazima yeye aongee ukweli ili mradi donda
ndugu liliopo katika muziki limepone.
"Wasanii
sisi ni ma-snichi sana aise, baada ya hii ishu ya Nandy ndio nimepata
uhakika. Wakati wa ishu ya Roma nilianza kuliona jinsi kwenye makundi
pembeni watu kibao walikuwa wanafurahi tena maneno kibao kama atakoma,
amezoea huyo. Jana na juzi nimekaa na watu wasanii wakubwa tu na wote
walikuwa wanasema bora limemtokea Nandy hili angalau spidi za 'show'
zitapungua", amesema Dogo Janja.
Pamoja
na hayo, Dogo Janja ameendelea kwa kusema.... ..."bora BASATA
ingemfungia miezi 6 apotee kidogo, walikuwa wanapiga stori kama utani
ila moyoni nimefikiria sana. Wasanii tuache roho mbaya, wote sisi
masikini tunahangaikia ugali. Tukipata ajali kazini, tusiombeane mabaya
tutafute amani".
Kwa
upande mwingine, Dogo Janja amewashauri wasanii wenzake wawe na moyo wa
upendo kwa wenzao na waache tabia ya kufurahia matatizo wanayowapata
wakiwa kazini.
Comments