Pongezi kwa mfungaji wa mabao hayo yote mawili, Nahodha John Raphael
Bocco ‘Adebayor’ moja kila kipindi na sasa Wekundi wa Msimbazi
wanafikisha pointi 49 baada ya kucheza mechi 21,
wakiwazidi kwa pointi
tatu mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 46 za mechi 21 pia.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa chipukizi Meschak Suda kutoka
Songea, aliyesaidiwa na Mohamed Mkono wa Tanga, hadi mapumziko Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bocco alifunga bao la kwanza kwa shuti la mguu wa kulia kufuatia
kuudondosha chini kwa kichwa mpira mrefu wa adhabu uliopigwa na beki
Yussuf Mlipili.
Bao hilo lilionekana kuwavuruga Njombe Mji FC na kujikuta wanawaruhusu Simba kutawala mchezo zaidi na kukaribia kufunga mara kadhaa.
Lakini dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika Simba wakiwa
mbele kwa hilo moja tu na kipindi cha pili hakukuwa na mabadiliko yoyote
kwa Njombe Mji FC kimchezo, kwani Wekundu wa Msimbazi waliendelea
kutawala mchezo.
Haikuwa ajabu Bocco tena alipowainua mashabiki wa Simba kushangilia
bao la pili baada ya kufunga vizuri dakika ya 64 kwa mguu la kulia
kufuatia pasi ya beki wa kulia, Shomari Kapombe.
Kocha Mfaransa, Pierre Lechantre akawaingiza wachezaji wawili,
majeruhi wa muda mrefu, beki Salim Mbonde na kiungo Mnyarwanda Haruna
Niyonzima kumalizia mchezo.
Comments