Benki
ya Dunia (WB) imekubali kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika
kukabiliana na athari za mafuriko zinazosababishwa na mvua kubwa
zinazonyesha kila mwaka katika Jiji la Dar es Salaam na kuleta madhara
makubwa hususan katika eneo la Jangwani jijini humo.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
(Mb) wakati akizungumza na ujumbe wa Benki ya Dunia ulioongozwa na
Mkurugenzi wa Benki hiyo kwa nchi za Tanzania, Somalia, Burundi na
Malawi Bi. Bella Bird, katika mikutano ya kipupwe inayoendelea mjini
Washington DC.
Dkt.
Mpango amesema kuwa Benki ya Dunia imekubali kusaidia kukabiliana na
mafuriko katika bonde la mto Msimbazi hasa katika eneo la kutoka
Magomeni Mapipa kwenda Faya na tayari Benki hiyo imeanza zoezi la
kutafiti eneo la Jangwani ili kuweza kuangalia namna nzuri ya kugharamia
uboreshaji wa mifereji katika bonde la mto Msimbazi ili kumaliza kero
hiyo kwa wananchi wa Dar es Salaam.
“Tumewaeleza
Benki ya Dunia changamoto hii ambayo imekuwa inajirudia kila mara na
kusababisha upotevu wa maisha ya watu, kusababisha kufungwa kwa
barabara, watu kushindwa kwenda kazini na wanafunzi kushindwa kwenda
shule, hivyo wameonesha nia ya kumaliza kero hii kwa wananchi,” alisema
Dkt. Mpango.
Amesema
kuwa baada ya timu ya Benki ya Dunia kumaliza kufanya kazi yao kwa
kushirikiana na Manispaa ya jiji la Dar es Salaam, Serikali inaamini
njia ya kudumu itapatikana na kuondokana na tatizo hilo la mafuriko ya
mara kwa mara katika eneo la Jangwani.
Mpekuzi.
Comments