Yanga imepangwa kucheza na Singida United kwenye mchezo wa robo fainali wa Kombe la Shirikisho(FA) huku Azam ikiangukia kwa Mtibwa Sugar katika michezo inayotarajia kufanyika kati ya Machi 30 na April Mosi.
Mechi nyingine zitakuwa kati ya Tanzania Prisons itakayokuwa mwenyeji wa JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya wakati Njombe Mji itakuwa ugenini kuikabili Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage Shinyanga.
Mchezo kati ya Yanga na Singida United ndio unaotarajiwa kuwa na mvuto zaidi kutokana na uimara wa vikosi vyote viwili vilivyosheheni wachezaji nyota na makocha wa kimataifa .
Timu hizo zimekutana mara mbili msimu huu,kwanza ilikuwa katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliofanyika Novemba 11 mwaka jana kwenye Uwanja wa Namfua Singida ambapo zilitoka suluhu.
Pia zikakutana tena Januari 8 mwaka huu kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Mapinduzi na kutoka sare ya bao 1-1.
Ukiacha mechi hiyo ya Kombe la FA pia timu hizo zitakutana tena katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Bara utakofanyika April 11 jijini Dar es Salaam.
RATIBA
Singida United vs Yanga
Prisons vs JKT Tanzania
Azam vs Mtibwa Sugar
Stand United vs Njombe Mji
Comments