Watu sita wapoteza maisha, nyumba milioni mbili Marekani zakosa umeme kwa sababu ya baridi kali, mafuriko.
Vifo hivyo vimeripotiwa kutokea Pennsylvania, Connecticut, Rhode Island, New York, Maryland, na Virginia, huku umeme ukikatika katika eneo kubwa linaloanzia North Carolina hadi Maine.
Magavana wa majimbo ya Maryland na Virginia wametangaza hali ya hatari huku askari wa gadi ya taifa wakitumika katika majimbo ya Massachusetts na Pennsylvania kutoa misaada. Maelfu ya watu wasio na makazi katika majimbo mbalimbali ya Marekani ni miongoni mwa walioathiriwa vibaya na hali hiyo ya hewa.
Tokea Ijumaa zaidi ya safari 4,000 za ndege zimefutwa katika maeneo mbalimbali ya Marekani huku baadhi ya safari zikiakhirishwa.
Aidha maeneo ya kusini mwa pwani ya Marekani yanakabiliana na kimbunga kikubwa kinachojulikana kwa jina la Nor’easter ambacho kimesababisha upepo mkali, theluji na mvua nzito nchini humo.
Marekani hukumbwa na vimbunga vya mara kwa mara lakini kimbunga cha mara hii kilichoandamana na theluji kali kimetajwa kuwa kibaya zaidi katika miongo ya hivi karibuni.
chanzo:parstoday.
Comments