Watu
tisa wanaodhaniwa kuwa ni wahamiaji haramu wamekamatwa na Jeshi la
Polisi Mkoani Mwanza kwa tuhuma za kuingia nchini Kinyume cha sheria.
Watuhumiwa
hao wamekamatwa katika eneo na Nyashishi Wilayani Msingwi Mkoani humo
wakiwa wamejificha katika vichaka kwa ajili ya kwenda kuchukuliwa kwa
ajili ya kuendelea na safari yao.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa kukamatwa kwa
raia hao kunafuatia taarifa za raia mwema aliewatilia shaka na kisha
kutoa taarifa kwa jeshi la polisi juu ya watu hao waliojificha katika
kichaka hicho.
Katika
hatua nyingine Kamanda Ahmed Msangi amewataka wananchi kutanguliza
uzalendo kwa kuwafichua watu wanaoshi nchini bila ya kuwa na vibali
maalumu na kinyume cha sheria.
chanzo:mpekuzi.
Comments