Watu 14 wauawa katika mlipuko wa bomu Mogadishu, Somalia.

Watu 14 wauawa katika mlipuko wa bomu Mogadishu, SomaliaKwa akali watu 14 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia mlipuko wa bomu uliotokea katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Duru za serikali ya Somalia zimetangaza kuwa, watu 14 wameuawa na makumi ya wengine wamejeruhiwa baada ya mlipuko wa bomu la kutegwa garini kutokea jana jirani na hoteli moja mjini Mogadishu.
Baadhi ya duru za hospitali zimetangaza kuwa, hali ya baadhi ya majeruhiwa wa mlipuko huo ni mbaya mno na kwamba, upo uwezekano wa kuongezeka idadi ya wahanga wa mlipuko huo wa jana. 
Kundi la wanamgambo wa al-Shabab limetangaza kuwa, ndilo lililohusika na mlipuko huo ambao umepelekea watu wasio na hatia kuuawa.
Wakati huo huo, jeshi la Somalia limetangaza kuwa, limewatia mbaroni maafisa wawili wa ngazi za juu wa kundi hilo la wanamgambo wa al-Shabab.
Kundi la al-Shabab lilikuwa likidhibiti maeneo ya katikati na kusini mwa Somalia lakini lilipokonywa maeneo hayo muhimu, ikiwemo miji mikubwa ambayo ilikuwa mikononi mwa wanachama wa genge hilo mwaka 2015 kufuatia operesheni kubwa zilizofanywa na jeshi la Somalia kwa kushirikiana na askari wa kusimamia amani wa Umoja wa Afrika (AMISOM). 
Tangu wakati huo kundi hilo limefanya mashambulizi ya kigaidi katika maeneo tofauti ya Somalia na hata katika ardhi ya nchi jirani.
Harakati za wanamgambo wa al-Shabab zimeifanya Somalia izidi kukabiliwa na ukosefu wa amani. 
chanzo:parstoday.

Comments