
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole amesema tukio hilo
lilitokea saa tano usiku wa Februari 28, 2018 na kuwataja watoto hao
kuwa ni Redia Elias (10), Modesta Elias (9), Steven Deogratias (9), na
Kizengela Elias (8).
Amesema wakati moto huo uliotokana na mshumaa kushika chandarua na
kuunguza godoro walilokuwa wamelalia, mama yao alikuwa amelala kwenye
nyumba nyingine ya familia hiyo.
“Watoto wote ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Pambalu na wanatarajiwa kuzikwa kesho,” amesema Kipole.
Mmoja wa majirani wa familia hiyo, Amas Juma amewataka wazazi kuwa
makini pale wanapolazimika kuwawashia watoto mishumaa kwa kuhakikisha
unazimwa kabla ya kulala.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema polisi
wanaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo na kutoa wito kwa wazazi na
walezi kuchukua tahadhari watoto wanapobaki wenyewe nyumbani.
Chanzo: Mwananchi na zanzibar24.
Comments