Wanawake wa Z’bar ongezeni juhudi katika kazi na muache kabisa kutegemea waume zenu.

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake  Zanzibar Tamwa  Dr Mzuri Issa  amewataka  wanawake nchini kuongeza juhudi  katika  kazi za uzalishaji wa bidhaa  kwani hatua hiyo itawasaidia  kuondokana na utegemezi  kwa waume zao.

Akizungumza na Zanzibar24 amesema  hivi sasa wanawake  wamekuwa na muamko wa kutosha katika  kujishughulisha na harakati za maendeleo, ambapo amesema hatua  hiyo imetokana na  elimu inayotolewa na chama cha waandishi wa habari wanawake Zanzibar tamwa pamoja na taasisi nyengine nchni zinazoshughulikia  masuala ya wanawake.

Hata hivyo  Dr Mzuri amesema  licha ya elimu wanazopewa wanawake katika kujishughulisha katika  harakati za maendeleo lakini tatizo kubwa linalowakabili wanawake wengi hivi sasa ni elimu ndogo  na wengine hawajasoma kabisa  hali inayowakwamisha katika kutangaza bidhaa zao.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara wa viwanda Dr.Mohammed Hafidhi amewataka  wajasiriamali wanaozalisha bidhaa nchni kuongeza thamani ya bidha zao kwa kuzifanyia ubunifu utakaowavutia wateja  kuweza kuzinunua ili wahakikishe wanazingatia suala la usafi wakati wanapotengeneza bidhaa hizo ili kulinda afya za walaji.

chanzo: Zanzibar24.

Comments