Ripoti zinasema kuwa, mamia ya familia za Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo zimekuwa zikihatarisha maisha yao kwa kupanda boti mkweche na zilizochakaa wakivuka maji ya Ziwa Albert na kuingia nchini Uganda.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, makumi ya familia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimekuwa zikiingia nchini Uganda kila siku zikikimbia machafuko yanayoshuhudiwa nchini kwao.
Wakimbizi wapatao 44,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanakadiriwa kuingia nchini Uganda hadi sasa tangu kkuanza mwaka huu wa 2018.
Wakimbizi hao wanasema kuwa, raia wengi wameuawa na mamia ya nyumba kuchomwa moto mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Aidha wakimbizi hao wanaowasili Uganda wanasema kuwa, wenzao wengi wamekusanyika katika ufukwe wa Ziwa Albert upande wa DRC wakisubiri kuingi nchini Uganda.
Baadhi ya mashirika yanalitaja wimbi hilo la wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaoingia nchini Uganda kuwa ni mgogoro mwingine wa wakimbizi na wahajiri baada ya ule unaoshuhudiwa hivi sasa huko nchini Libya.
Hivi karibuni Filippo Grandi, Kamishna Mkuu wa Shrika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), aliiipongeza serikali ya Uganda kwa sera nzuri inayowaenzi na kuwathamini wakimbizi wanaoingia katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
chanzo:parstoday.
Comments