Waingereza wapinga bin Salman kufanya safari London; wasema ni mtenda jinai.

Waingereza wapinga bin Salman kufanya safari London; wasema ni mtenda jinaiWananchi wa Uingereza wameendelea kupinga safari ya Muhammad bin Salman mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia mjini London wakisema kuwa, viongozi wa nchi hiyo wanapaswa kufuta safari ya bin Salman kutokana na kutenda kwake jinai huko Yemen.

Wananchi hao wameanzisha mpango wa kukusanya saini ambapo wameashiria jinai za utawala wa Saudia dhidi ya wananchi wa Yemen na  na kusisitiza kwamba, Muhammad bin Salman hapaswi kutia mguu wake nchini Uingereza.
Wapinzani wa safari ya bin Salman huko London wameanza kukusanya saini katika mtandao wa Intaneti wa Bunge la nchi hiyo ambapo wanamtaka Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, afute mwaliko wake kwa Muhammad bin Salman wa kufanya safari katika mji mkuu wa nchi hiyo London.
Inaelezwa kuwa, Wabunge wa Bunge la Uingereza wanamtambua Bin Salman kuwa amefanya jinai kubwa katika vita vya Yemen ambayo vimesababisha maafa makubwa zaidi ya kibinadamu nchini humo. 
Vile vile wabunge hao wanasema asilimia zaidi ya 70 ya kesi za kunyongwa watu nchini Saudi Arabia zimetokea baada ya Muhammad bin Salman kushika mamlaka ya nchi hiyo. 
Itakumbukwa kuwa, mwezi uliopita, safari iliyopangwa kufanywa na Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia nchini Uingereza iliakhirishwa kwa muda usiojulikana baada wabunge, jumuiya za kiraia na makundi ya kutetea haki za binadamu kupinga safari hiyo.
Wabunge wasiopungua 17 wa vyama tofauti vya siasa nchini Uingereza wametia saini waraka wakimtaka Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Theresa May kufuta safari ya Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia, Muhammad bin Salman mjini London.
chanzo:parstoday.

Comments