Velayati: Uingereza ilizembea katika kadhia ya kuhujumiwa ubalozi wa Iran mjini London.

Velayati: Uingereza ilizembea katika kadhia ya kuhujumiwa ubalozi wa Iran mjini London Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema serikali ya Uingereza ilizembea katika majukumu yake wakati wa kuhujumiwa ubalozi wa Iran mjini London.

Ali Akbar Velayati, Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa Jumamosi aliwaambia waandishi habari mjini Tehran kuwa: "Bila shaka serikali ya Uingereza inabeba jujumu la kulinda  ofisi za kidiplomasia nchini humo, ukiwemo ubalozi wa Iran majini London. 
Serikali ya Uingereza ilizembea katika kuwazuia wahuni kadhaa waliouhujumu ubalozi wa Iran."
Velayati amoengeza kuwa, waliouhujumu ubalozi wa Iran mjini London wana uhusiano na baadhi ya mirengo nchini Uingereza.
Naye Mohammad Jawad Larijani Mkuu wa Idara ya Haki za Binadamu katika Vyombo vya Mahakama Iran amesema ubalozi wa Iran mjini London ulihujuiwa kwa ushirikiano na polisi ya Uingereza. 
Amesema serikali ya Uingereza inapaswa kubeba dhima ya kitendo hicho kiovu.
Itakumbukwa kuwa Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini London adhuhuri ya  Ijumaa ulishambuliwa na kundi moja la watu wanaojiita wafuasi wa kundi la mrengo wa Shirazi.
Bahram Qassemi Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Ijumaa usiku alisema waliohujumu ubalozi wa Iran mjini London wamekamatwa.
Pote la Shirazi ambalo pia linatajwa kuwa ni "Mashia wenye kupata himaya ya Uingereza" linaongozwa na mtu anayejulikana kama Sadeq Shirazi. 
Hilo ni pote ambalo pia huyavunjia heshima matukufu ya Waislamu wa Ahlu Sunna.
chanzo:parstoday.

Comments