Trump ataka Marekani iwe na 'rais wa maisha kama China'.

Trump ataka Marekani iwe na 'rais wa maisha kama China'Rais Donald Trump wa Marekani ametoa matamshi yanayoashiria kuwa angependa kuiona nchi hiyo ikiwa na rais wa kudumu maisha.

Akihutubu katika jimbo la Florida Jumamosi, Trump amesema angependa Marekani iwe na rais wa maisha kama China.
Trump amempongeza Rais wa China, Xi Jinping, baada ya chama chake tawala cha Kikomunisti kutangaza mpango wa kufuta kikomo cha mihula miwili cha kuwania urais.
Wadadisi wa mambo wanasema hatua hiyo inalenga kumuondolea kizuizi Jinping na yumkini akaendelea kuongoza kwa kipindi kirefu.
Televisheni ya CNN imemnukuu Trump akisema, "Mtizame rais wa China, kiwepesi amefanikiwa kuwa rais wa maisha, ninadhani ni jambo adhimu sana. Ninatamani siku moja Marekani pia iwe na rais wa kudumu milele."
Licha ya Trump kumpongeza Rais wa China mara kwa mara, lakini amekuwa akikosoa vikali sera za kibiashara za nchi hiyo, sambamba na kutishia kuiadhibu nchi hiyo ya bara Asia kwa kile anachokitaja kama 'wizi wa hatimiliki'.
chanzo:parstoday.

Comments