Mwanamuziki
wa Bongo fleva Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka na kukiri haoni
ubaya wa yeye kukata mauno stejini maana yupo kazini.
Suala
limekuwa ishu baada ya video yake akiwa anatumbuiza stejini huku
anakata mauno kihasara hasara stejini kusambaa Kwenye mitandao ya
kijamii.
Ndipo
watu kuanza kuhoji inakuwaje mke wa mtu anafanya mambo yake hadharani
lakini Shilole amewazima watu hao na kusisitiza kuwa Mume wake anajua
anachofanya hivyo haoni kama kuna tatizo.
Shilole
amefunguka alipohojiwa na Global Publishers kuhusu hilo na kuweka wazi
kuwa anawashangaa watu wanaozungumza kuhusu hilo wakati wanajua wazi
kuwa ile ndio kazi yake na mume wake Uchebe analitambua hilo hivyo hana
neno juu ya hilo.
"Mume
wangu Uchebe (Ashraf) anajua nikiwa kazini, chochote naweza kufanya
jukwaani, haoni shida maana ananipenda na kazi yangu hivyo wanaosema
ninawasihi waache kwani pale nilikuwa kazini kwa hiyo lazima
niwapagawishe mashabiki wangu”.
Comments