Real Madrid, Liverpool zatangulia robo fainali Ulaya.

KLABU za Real Madrid na Liverpool zimefuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kufuatia matokeo yao mazuri ya mechi za marudiano zilizochezwa juzi.

Ikiwa ugenini nchini Ufaransa,Real Madrid iliwalaza wenyeji PSG magoli 2-1 huku Liverpool ikilazimishwa sare 0-0 katika uwanja wa Anfield.

Cristiano Ronaldo alifunga bao lake la 12 kwenye michuano hiyo kabla ya Casemiro kuongeza la pili huku lile la kufutia machozi la PSG likifungwa na Edinson Cavanni.

Sare ya bila ya kufungana nayo iliwapeleka Liverpool robo fainali huku golikipa wa FC Porto Iker Casillas akiweka rekodi katika mchezo huo kwa kuwa kipa wa kwanza kucheza na Liverpool katika ligi hiyo msimu huu bila ya wavu wake kuguswa.(AFP)

Comments