Mbunge
wa Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye amesema ulevi wa baadhi ya viongozi
wa Afrika kutamani na kubadili ukomo wa wao kuwa madarakani ni ushetani.
Kupitia
ukurasa wake wa twitter leo Machi 5, 2018, Nape ameandika kuwa ni
lazima ushetani huo upingwe kwa nguvu zote hasa na vijana kabla haujaota
mizizi na kusambaa.
Nape
ambaye amewahi kuwa waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla
ya kuvuliwa wadhifa huo na Rais John Magufuli na nafasi yake
kuchukuliwa na Dk Harrison Mwakyembe amekiri kuwa twitter ni yake ingawa
hakuwa tayari kufafanua zaidi.
“Huu
ulevi wa baadhi ya viongozi wa Afrika kutamani na kubadili ukomo wa wao
kuwa madarakani ni ushetani na lazima upingwe kwa nguvu zote hasa na
vijana kabla utaratibu huu haujaota mizizi na kusambaa! Hii ni zaidi ya
kansa!” unasema ujumbe huo wa twitter.
chanzo:Mpekuzi.
Comments