Sambamba na kukosoa vikali hatua ya kuendelea kushikiliwa katika kifungo cha nyumbani mwanazuoni huyo wa Waislamu wa Shia nchini Bahrain, Muqtada Sadr amezitaka asasi za kimataifa kuingilia kati suala hilo na kuhitimisha mara moja kifungo hicho cha kidhalimu.
Kadhalika kiongozi huyo wa Harakati ya Sadr ya nchini Iraq ametaka kuachiliwa huru wafungwa wote wa kisiasa wanaoshikiliwa katika korokoro za utawala wa Aal-Khalifa.
Wakati huo huo Sayyid Muqtada Sadr amekemea kitendo cha utawala wa Bahrain cha kuwavua uraia wananchi na amesisitizia udharura wa kufikiwa malengo ya wananchi wa taifa hilo wanaodhulumiwa kila uchao.
Inafaa kuashiria kuwa, utawala huo wa kiimla mbali na kumvua uraia Sheikh Sheikh Issa Qassim, mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu nchini Bahrain mwezi Juni mwaka 2016, uliamuru askari wake kuzingira eneo la Diraz, ambalo ndipo yalipo makazi ya mwanazuoni huyo mtajika.
Katika uwanja huo, utawala huo na kwa lengo la kutaka kumuua, ulizuia kiongozi huyo wa kidini kupatiwa matibabu katika hospitali nje ya nyumba yake suala ambalo lililaaniwa vikali na jamii mbalimbali ndani na nje ya nchi hiyo.
Hadi sasa Sheikh Issa Qassim, ametimiza siku 300 za kizuizi cha nyumbani alichowekewa na utawala huo wa kiimla wa Aal Khalifa katika hali ambayo angali anasisitiza kutumika njia za amani katika kuendelezwa vuguvugu la mapinduzi ya wananchi.
chanzo:parstoday.
Comments