Msafara
wa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Hamphrey Polepole umepata ajali
katika eneo la Kijiji cha Nyamidato, Kata ya Makere wilayani Kasulu
mkoani Kigoma.
Ajali
hiyo imehusisha gari aina ya Toyota Vx yenye namba za usajili T150 CWE
iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja la Kibuta
wakati wakielekea katika ziara ya kiongozi huyo wilayani Kakonko, mkoani
humo.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa
ajali hiyo na kueleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni kupasuka kwa
gurudumu la nyuma upande wa kulia.
Kwa
mujibu wa Kamanda Otieno, waliojeruhiwa ni pamoja na Katibu wa CCM mkoa
Naomi Kapambala, Mwenyekiti wa UVCCM Sylivia Sigura pamoja na Katibu
Mwenezi, Feruz ambao wamekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Kibondo
kwa matibabu.
Polepole
amewasili mkoani Kigoma na kupokelewa wilayani Uvinza akitokea mkoani
Tabora ambapo atakuwa Kigoma kwa takribani siku tatu.
chanzo:Mpekuzi.
Comments