Mifumo iliyopo na sera ibadilishwe wanawake waweze kufika katika dira ya maendeleo 2020.

Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  itaendelea kuwaunga mkono wanawake wa makundi yote wanaojishughulisha na  kazi za ujasiriamali   kwa kuwawezesha  kuwapatia mitaji na kuwasaidia kuwatafutia masoko ya kuuzia biashara zao kwani ndio kikwazo kikubwa kinachowakabili wajasiriamali nchini.
Akizungumza katika Shamrashamra za maadhimisho ya kuelekea katika siku ya wanawake duniani huko Ngomekongwe amesema  serikali inatambua kuwa wanawake wajasiriamali wanakabili na matatizo mbalimbali licha ya kuwa na muamko wa kujiunga na vikundi mbalimbali vya kujiendeleza kiuchumi ambapo  amewataka  kutovunjika moyo kwani sera zilizopo zitaweza kuwanyanyua  wanawake katika kufikia dira ya maendeleo nchini.
Amesema mashirikiano  baina ya wajasiriamai , serikali pamoja na wadau wa maendeleo ni jambo litakalo saidia kufikia uchumi wa kati na kuweza kukuza gurudumu la maendeleo  lakini pia kujitengemea wenyewe bila ya kuwa utegemezi kutoka serikalini.
Aidha Balozi Amina  amezitaka taasisi mbalimbali zinazosimamia masuala ya wanawake kuhakikisha kuwa mifumo  yote iliyopo  ya  maendeleo inakuwa rafiki na inalenga katika kuyaendeleza makundi yote ili kufaidika na  mipango ya maendeleo kama  ilivyodhamira ya serikali ya kufikia uchumi wa kati wa viwanda.
Amesema Ujio wa viwanda vidogovidogo na kati Zanzibar vitawasaidia  wananchi wengi hasa wafanyabiashara za wajasiriamali kuuza bidhaa zao kwa urahisi na hatua hiyo inawawezesha kuzalisha bidhaa zao kwa wingi na vyenye ubora.
Mapema Mkurugenzi Jumuiya ya waandishi wa habari wanawake Zanzibar tamwa Dr Mzuri issa amesema  lazima serikali iwaunge mkono wanawake ili kuondoka katika mifumo dume ya utegemezi kwani hali hiyo itawasaidia kutodhalilishwa na waume zao pamoja na wao kukomboka katika hali gumu ya maisha.
Hata hivyo Mzuri amesema elimu bado inahitajika  kwa wananchi juu ya kuona umuhimu wa kutumia bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wa ndani kwani hatua hiyo inasaidia kukuza soko la ndani ya nchi.
Amesema tayari wanawake wengi hivi sasa wameelimika katika masuala ya ujasiriamali pamoja na kuwa na muamko wa kumiliki ardhi lakini wanarudishwa nyuma na baadhi ya taasisi kutowapa mashirikiano mazuri pindi wanapohitaji huduma au msaada kutoka kwao hivyo serikali ihakikishe inasimamia watendaji wake ili kuona changamoto hizo zinaondoka kwani ndio miongoni mwa vikwazo  vinavyopelekea wanawake kushindwa kufikia malengo yao.
Kwaupande wake Msoma Risala  katika Maadhimisho hayo kwa niaba ya wanawake wa Zanzibar Jina Pandu amesema kukosekena  kwa malighafi za uhakika za kuzalisha bidhaa zao  itapelekea wao kushindwa kuzalisha vizuri bidhaa zenye ubora hivyo serikali ihakikishe inawasaidia  wajasiriamali  ili kuweza kupata malighafi kwa urahisi.
 Hata hivyo amesema kukosekana kwa mashirikiano kwa baadhi ya taasisi za serikali  kunachangia kuduma uzalishaji wa bidhaa zao  hasa taasisi zinazotoa huduma za maji safi na salama zawa pamoja na taasisi zinazotoa huduma za umeme zeco zinawarudisha nyuma kwani wakikosa  huduma hizo hushindwa kufanya shughuli zao.
Wakati huo huo wametoa wito kwa serikali kuziomba mamlaka zinazohusika na kukusanya mapato  kuwapunguzia kodi wajasiriamali wadogo kwani wanashindwa kumudu gharama za kodi kutokana mitaji yao ni midogo ukilingamishwa  kodi wanazotozwa.
Maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yanatarajiwa kuadhimishwa tarehe 8 ya mwezi Murch  mwaka huu ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Tubadilishe mifumo  iliyopo na sera  ili wanawake wote wafaidike  na maendeleo ya kiuchumi,kijamii na kisiasa.
chanzo:Zanzibar24.

Comments