Mafundi seremala walia na tatizo la mbao.

seremalaUkataji misitu kiholela na uchomaji miti umechangia kuwapa ugumu mafundi wa uchongaji zanzibar kushindwa kupata mbao kwa ajili ya kazi zao za ujasiriamali .

Wakizungumza   baadhi ya Vijana  wanaojishughulisha na fani ya uchongaji wamesema  licha ya kuitumia fursa ya kujiajiri wenyewe ili kuondokana na tatizo la ajira  lakini bado katika fani hiyo wanakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa mbao kwa ajili ya kutengezea  vifaa vya matumizi ya nyumbani na maofisini.

Wamesema  hivi sasa vijana wengi wamekuwa na muamko wa kujifundisha fani mbalimbali ili kuweza kujiajiri lakini wanakabilia na tatizo la mitaji na vifaa vyenye ubora kufanikisha kazi zao ili kuweza kuwaingizia  kipato.

Wamesema mbali na yote lakini  tatizo la kuadimika kwa miti inayotumika kwa ajili ya mbao  inawapa ugumu katika kazi zao za uchongaji hivyo serikali imeombwa  kuwasaidia wananchi hasa vijana walijishughulisha katika  fani hiyo kuweza kuwapunguzia ushuru pindi wanapokwenda kununua mbao nje ya Zanzibar.

Aidha  mafundi  hao wamewataka vijana kutovunjika moyo katika kufanya kazi licha ya kuwa bado kuna changamoto nyingi zinazopelekea  kuwakwamisha lakini  wavumilie ili kuweza kupata riski za halali.

chanzo: Zanzibar24.

Comments